Saido: Ishu yangu na Simba ipo hivi



KIUNGO mshambuliaji aliyekuwa akikipiga Yanga, Said ‘Saido’ Ntibazonkiza amevunja ukimya na kueleza mustakabali wake kwa msimu ujao, huku akifunguka kila kitu juu ya ishu yake ya kutakiwa kuvaa uzi wa rangi nyeupe na nyekundu wa vijana wa Msimbazi, Simba.

Mashabiki wa Simba wameanza kuwatambia wenzao wa Yanga wakiwaambia “hamtaamini” baada ya kusikia kwamba mabosi wao wanamnyatia Saido na nyota huyo wa Burundi amezungumza na Mwanaspoti na kuanika kila kitu kilichopo juu ya dili la Msimbazi.

Saido aliachana na Yanga baada ya kuimaliza mkataba wake mwishoni mwa mwezi uliopita na sasa ni mchezaji huru na tayari mabosi watatu wa Simba walishawasiliana naye kwa vipindi tofauti na kumuwekea mkataba wa mwaka mmoja mezani.

Mwanaspoti linafahamu kuwa, Simba ilitaka kumsajili kwa mkataba huo mfupi, lakini naye aliweka masharti ikiwamo kutaka kipengele kitakachompa uhuru wa kutimka akipata timu nyingine, mbali na kupata nafasi ya kucheza kikosini.


 
Hata hivyo, mazungumzo ya pande hizo mbili hayakupata muafaka kwani mabosi walikuwa wanakuna kichwa juu ya sharti ya kupata wasaa mkubwa wa kucheza na kutimka akipata timu, japo Mwanaspoti linafahamu jamaa(Saido) ana ofa kutoka klabu mbili za Arabuni, Qatar na Saudi Arabia.

Akizungumza na Mwanaspoti, Saido alikiri kufuatwa na viongozi wa Simba sambamba na timu nyingine ikiwemo Singida Big Stars na kuweka wazi kuwa hadi sasa hajaamua wapi asaini.

“Zimekuja ofa nyingi mezani, wote hao unaowataja (Simba na Singida) nimeongea nao tu, ila sijasaini kokote. Kila upande kuna sababu zake na viongozi wa timu hizo wanazijua na huenda wanazifanyia kazi,” alisema Saido na kuongeza:


“Sitaki kuliongelea sana hili, tusubiri kwanza kila kitu kikamilike mtaambiwa wapi nitacheza msimu ujao.”

Kiungo huyo aliyeifungia Yanga mabao saba na asisti nne msimu huu, huku akiwa mmoja ya nyota walioisaidia timu hiyo kuganda kileleni kwa muda mrefu na kubakisha hatua chache ya kutawaza ubingwa, ikiwa ni baada ya kulisotea taji kwa misimu minne mfululizo mbele ya Wekundu wa Msimbazi.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad