Serikali Kufuta Ada Kidato cha Tano, sita



Wanafunzi wa kidato cha sita walipokuwa wanafanya mtihani
SERIKALI ya Tanzania imetangaza kusudio la kufuta ada kwa wanafunzi wa kidato cha tano na sita, katika mwaka wa fedha ujao wa 2022/23. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Hayo yamelezwa leo Jumanne, tarehe 14 Juni 2022, bungeni jijini Dodoma na Waziri wa Fedha na Mipango, akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Serikali kwa mwaka wa fedha wa 2022/23.

“Kwa sasa tuna takribani wanafunzi 90,825 wa kidato cha tano na 56,880 wa kidato cha sita. Mahitaji ya fedha ni takribani Sh. 10.3 bilioni. Ili kuwapunguzia gharama watoto hawa, napendekeza kufuta ada ya wanafunzi wa kidato cha tano na sita,” amesema Dk. Mwigulu.


Dk. Mwigulu amesema, kufuatia hatua hiyo, elimu bila malipo itaanza katika shule ya msingi hadi kidato cha tano na sita.


Aidha, Dk. Mwigulu amesema, Serikali inaangalia namna ya kusaidia wanafunzi wa vyuo vya kati, pindi hali ya uchumi wa nchi itakavyokuwa imetengemaa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad