Simba SC: Hatuna mpango na Luis Miquissone




Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba SC Mulamu Nghambi amesema klabu hiyo haina mpango wa kumsajili kwa mkopo Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Msumbiji na klabu ya Al Ahly ya Misri Luis Miquissone kama inavyoelezwa.

Simba SC inatajwa na kupewa nafasi kubwa kumsajili Miquissone mwishoni mwa msimu huu, kufuatia kiungo huyo kuwa na mazingira magumu ya kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha Al Ahly tangu aliposajili mwezi Julai mwaka 2021.

Mulamu amesema Simba SC haijatuma Ofa ya kumsajili Miquissone kwa mkopo, na taarifa za kufanya hivyo wanaziona kwenye Mitandao ya Kijamii, lakini ukweli ni kwamba hawana mpango huo.

Amesema azimio hilo linatokana na ugumu wa kumpata mchezaji aliye kwenye vikosi vya klabu kubwa Barani Afrika, huku akizitaja kuwa ni Al Ahly, Zamalek, Wydad Casablanca, Kaizer Chief, Orlando Pirates na nyinginezo.


 
“Ngumu kwa sasa kumpata mchezaji anayecheza timu kubwa zilizopo katika Ukanda wa Afrika, hapo nazuzungumzia Al Ahly, Zamalek, Wydad Casablanca, Kaizer Chiefs na nyinginezo.

“Hivi sasa Luis ameanza kupata nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza, hivyo ngumu kumpata kirahisi kama watu wanavypofikiria.”

“Labda itokee lakini hadi hivi sasa bado hatujapata taarifa rasmi za kiofisi kutoka Al Ahly juu ya Luis kutolewa kwa mkopo,” amesema Nghambi.


Miquissone huenda akaondoka Al Ahly, kufauatia Kocha Pitso Mosimane aliyemsajili akitokea Simba SC kuondoka klabuni hapo usiku wa kuamkia jana Jumanne (Juni 14), hivyo Kocha ajaye anaweza akashindwa kumtumia kwenye mipango yake.

Miquissone alisajiliwa Al Ahly, baada ya kuonesha uwezo mkubwa akiwa Simba SC kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika msimu uliopita 2020/21.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad