Rais wa Shirikisho la soka barani Afrika (CAF) Patrice Motsepe.
Rais wa Shirikisho la soka barani Afrika (CAF) Patrice Motsepe. © AFP / Daniel Beloumou Olomo
Shirikisho la soka barani Afrika CAF limetangaza kuwa Tanzania itakuwa mwenyeji wa mkutano mkuu wa kawaida wa shirikisho hilo, utaoafanyika tarehe 10 mwezi Agosti.
CAF imesema mkutano huo wa 44 utafanyika katika jiji la Arusha, Kaskazini mwa nchi hiyo.
Mkutano huo utahudhuriwa na viongozi wa vyama wa soka barani Afrika na wadau wengine mbalimbali, kujadili maendeleo na changamoto za mchezo huo barani Afrika.
Kenya na Zimbabwe, zimefungiwa na Shirikisho la soka duniani baada ya serikali zao, kuingilia masuala ya uongozi wa mchezo huo, kinyume na kanuni ya FIFA.
Mkutano mkuu wa 43 uliofanyika mwaka uliopita, ulifanyika jijini Rabat nchini Morocco.