''Wakati tukiwa wadogo nilikuwa nikiona Mtu akitaka kupika maharage lazima ayachambue. Wakati wa kuchambua yale yanayoonekana kwa macho ni mabovu hutupwa na yale yanayoonekana mazima hupikwa na kuliwa.
''Lakini cha kushangaza, hayo mengine yaliyoonekana ni mabovu mvua ikinyesha huota na kuchanua na Mama alitwambia "ngo'a tu hayo majani lakini hayo maharage yaliyochanua na kupendeza yawekee udongo yachanue zaidi"
Vivyo hivyo katika maisha, watu wanaweza wasione thamani yako kulingana na hali na mwonekano wako wa sasa na mazingira yanayokuzunguka. Watu wanaweza wakakubagua, wakakutenga na kukutupa kwa kukuona hufai kwa kuangalia hali uliyonayo kwa sasa.
Brother, sister hutakiwi kubishana nao, kaa kimya baraka zako zikianza kukujia watakuona jinsi unavyochanua na kupendeza kama maharage mabichi yaonekanayo yakupendeza yakiwa shambani.
Hali uliyonayo kwa sasa hivi niya mda tu, na wala haitachukua mda mrefu, hakika yake utachanua tu ila endelea kutenda yampendezayo Mwenyezi Mungu.🙏🏽
#getwellsoonmyhubby❤️'' @mke_wa_profjize