Unaambiwa Yanga Yakusanya Bilion1.07, Kutoka Kwa Wanachama Wake

 


Klabu ya Yanga ya Dar es salaam imetangaza kusajili wanachama 34,650 katika kipindi cha miezi 6 tangu zoezi hilo la kusajili wanachama wa klabu hiyo lilipoanza. Mkoa wa Dar es salaam ndio mkoa ulioongoza kwa kusajili wanachama wengi.

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Kilinet Mohammed Saleh ametangaza klabu ya Yanga kusajili idadi hiyo ya wanachama kupitia Mfumu wa kisasa wa Digital.


"Ndani ya kipindi cha miezi 6 tumeweza kusajili Wanachama 34,650 na kukusanya mapato ya Tshs Bilioni 1.07" amesema Mohammed Saleh


Kwa mujibu wa takwimu walizozitangaza hii leo klabu hiyo imetoa orodha ya mikoa ambayo imeongoza kwa kusajili wanachama wengi ambapo mkoa wa Dar es salaam ndi umeongoza ukiwa na wanachana 12,124, ukifuatiwa na Mwanza 1,982, Mbeya 1,655, Dodoma 1,521, Morogoro 1,410 na mkoa wa Pwani umesajili wanachama 1,341.


Kwa upande mwingine msemaji wa klabu hiyo Haji Manara amesema zoezi linalofuata ni utoaji wa kadi za mashabiki wa klabu hiyo ambazo gharama yake itakuwa Tsh 17,000/= ambapo mshabiki atapata Kadi ambayo itamuwezesha kuingia Uwanjani na pia punguzo la Bidhaa mbalimbali za Yanga SC kwenye maduka washirika wa Yanga SC

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad