Vitambilulisho vya NIDA Vitakavyo Isha Muda Kulipiwa Elfu 20



Vitambulisho vya Taifa vilivyotolewa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), 2013 vitaisha muda wake mwakani 2023 ambapo gharama za kupatiwa Kitambulisho kipya dhidi ya kilichopotea au kuharibika ni Shilingi 20,000 kwa awamu ya kwanza.

Hata hivyo kwa mujibu wa tovuti ya NIDA usajili wa awali unaonesha hauna tozo, ingawa hofu ya Wananchi wengi ni juu ya utaratibu wa upatikanaji wa vitambulisho hivyo wa jinsi vinavyochukua muda mrefu pasipo uhakika wa kukipata.

“Japo hali ni ngumu lakini itatulazimu kulipia hiyo pesa hakuna jinsi lakini hofu yangu ni kuhusu upatikanaji wake umekuwa ni mgumu sana hata sijui wanakwama wapi,” alisema mmoja wa wananchi Martha Mbuto mkazi wa Makole Jijini Dodoma.

NIDA kupitia tovutu yake inaonesha gharama za kupata kitambulisho kipya kwa awamu ya pili dhidi ya kilichopotea, kuharibika au kuharibiwa ni Shilingi 30,000 kwa awamu ya pili na 50,000 kwa awamu ya tatu na zaidi.


Juni 8, 2022, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni alisema vitambulisho vya Taifa vipo mbioni kutolewa baada ya kukamilika kwa mchakato wa makubaliano kati ya Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) na kampuni ya utengenezaji wa kadi hizo.

Masauni aliyasema hayo wakati akiongea na wananchi wa Biharamuro mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, na kuelezea malalamiko ya Wananchi juu ya kukosekana kwa vitamabulisho hivyo kwa mchakato wake kuchukua muda mrefu.

“Wananchi wamekuwa wakilalamika sana na hasa maeneo ya mipakani lakini jitihada za Rais zinaonekana kwani ametupatia pesa ili kukamilisha vitambulisho, na tayari NIDA imesaini mikataba na kampuni yenye tenda ya utengenezaji wa kadi hizo,” amesema Masauni.


Alisema Wizara itahakikisha jambo hilo linamalizika kwa ufanisi baada ya Rais Samia kutoa Shilingi Bilioni 42.5 za kununua kadi ghafi zitakazokamilisha zoezi la utengenezwaji na ugawaji wa vitambulisho hivyo kwa wananchi.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad