Naibu Spika wa Bunge Mussa Zungu, amewaonya wabunge wenye tabia za kuingilia wenzao wanapokuwa wanachangia ama kuuliza maswali na kutaka tabia ya kung'ang'ana na neno taarifa linakoma mara moja kwani wanawatoa kwenye reli wachangiaji.
Kauli hiyo ameitoa hii leo Juni 13, 2022, wakati akisitisha shughuli za Bunge hadi kesho saa 3:00 asubuhi, na kusema mara baada ya Bajeti Kuu ya serikali hakutakuwa na taarifa zisizo na msingi, kwani taarifa nyingi zimekuwa hazina maana.
"Waheshimiwa wabunge tumeona katika mijadala mbalimbali ndani ya Bunge letu, wabunge wengi tuna tabia ya kusitisha mchangiaji kwa kutoa taarifa na taarifa nyingi hazina msingi mna tabia ya kuharibu flow ya mtu aliyepewa muda mfupi kuchangia mambo ya msingi halafu wewe unasimama taarifa tena unakuwa king'ang'anizi taarifa, taarifa, halafu unasimama unasema hata jimboni kwangu ni hivyo hivyo kanuni zetu haziruhusu,"amesema Naibu Spika