Wakili wa kina Mdee atoa kauli kifuatacho




WAKILI Aliko Mwamanenge anayeongoza jopo la mawakili wa kina Halima Mdee kupinga kufutwa uanachama wa CHADEMA, amesema bado hawajachukua hatua zozote kutokana na uamuzi wa juzi wa Mahakama Kuu kuhusu shauri hilo.

Juzi, Mahakama Kuu Masijala Kuu iliyaondoa maombi ya waliokuwa wanachama 19 wa CHADEMA baada ya kubaini yana upungufu wa kisheria.

Wakili Mwamanenge alipotafutwa jana kuzungumzia hatua zinazofuata baada ya maombi yao kutupwa, alisema jana jioni walikuwa hawajachukua hatua yoyote na walikuwa wanasubiri kuteta na wateja wao.

Wakati hali ikiwa hivyo kwa kina Mdee, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema muda mfupi baada ya mahakama hiyo kutoa uamuzi wa shauri hilo, kiliandika barua kwa Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson, ili atekeleze ile barua yake ya awali waliyomwandikia.

Wabunge hao 19 wanaoongozwa na Mdee, walifungua maombi hayo mahakamani huko kuomba mahakama itoe kibali cha kufungua kesi ya kupinga mchakato uliowavua uanachama wa CHADEMA.


 
Pia waliomba mahakama iweke zuio la kutokuchukuliwa kwa hatua zozote dhidi yao hadi pale maombi yao ya msingi yatakapoamuliwa.

Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Zanzibar, Salum Mwalimu, alipozungumza na waandishi wa habari mkoani Dar es Salaam jana, alisema wajibu wao mkubwa ni kuhakikisha taarifa ya hukumu hiyo inafika kwa Spika wa Bunge.

“Tayari tumeshafanya hivyo, tumemwandikia barua jana (juzi) jioni mara baada ya hukumu na kuituma kwa barua pepe inayotumiwa na Bunge, kupitia Katibu wa Bunge kumwelezea hukumu ile na kumtaka Spika wa Bunge kutekeleza barua ya CHADEMA ya Mei 12 mwaka huu kwa mujibu wa Ibara 71 (1) kifungu kidogo (f) ya Katiba ya mwaka 1977 kama ilivyokuwa imeshauriwa na chama.


Mwalimu alisema barua hiyo ni yenye namba C/HQ/ABM/PARL/33/38 ya Juni 22 mwaka huu iliyotiwa saini na Katibu Mkuu CHADEMA, John Mnyika, na nakala kupelekwa kwa Msajili wa Vyama vya Siasa na Mkurugenzi wa Uchaguzi kwa ajili ya taarifa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad