Wanafunzi Washauriwa Kusomea Ubaharia



SHIRIKA la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limetoa ushauri kwa wanafunzi kusomea taaluma ya ubaharia ili iwasaidie kuondokana na tatizo la ajira.

TASAC, Baharia Gabriel Manase.
Kauli hiyo ilitolewa leo na Mkurugenzi wa Udhibiti wa Usalama na Ulinzi wa vyombo vya usafiri majini na utunzaji wa mazingira kutoka TASAC, Baharia Gabriel Manase, wakati akiwasilisha mada kwenye semina ya wahariri na waandishi wa habari Bagamoyo mkoani Pwani.

Amesema sekta ya ubaharia kwa sasa ina fursa kubwa ya ajira tofauti na watu wanavyodhani.

"Vijana wengi wanaona sekta hii ya ubaharia ni ya kihuni, nataka niwaambie kwamba, kati ya sekta zenye fursa kubwa ya ajira ni pamoja na hii na ina wasomi wazuri sana.Mwaka jana kuna fursa kubwa ilipatikana ya kupeleka mabaharia kwenda kufanya kazi nje ya nchi, kwa hiyo walikwenda," amesema Manase na kuongeza;

"Na mpaka sasa bado mabaharia wanahitajika kwa wingi, kwa hiyo niwaombe vijana na wanafunzi wasomee hii sekta ina fursa kubwa. Kipindi cha COVID-19, mahabaria zaidi ya 400 walikuwa wanahitajika kwenda kufanya kazi nje ya nchi."


Amesema miaka ya nyuma sekta hiyo ilikuwa inaonekana si nzuri kusomea na kwamba ni vema vijana na wanafunzi wakabadilisha mawazo yao na kwenda kusomea ili waondokane na tatizo la kukosa ajira.

Manase, amesema bado lipo hitaji kubwa katika sekta hiyo hususani kwa mabaharia katika meli za kimataifa na hivyo kusisitiza vijana kujitokeza zaidi kusoma fani hiyo yenye ajira nyingi Duniani.

Amesema zipo kampuni nyingi za ndani na nje ya nchi ambazo zimekuwa zikihitaji mabahari kwa ajili ya kufanya nao kazi.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad