Watu 18 Wamefariki Wakijaribu Kuvuka Kuingia Uhispania



Wahamiaji 18 wamefariki na wengine kujeruhiwa wakati umati mkubwa ulipojaribu kuvuka eneo la Melilla nchini Uhispania Kaskazini, maafisa kutoka nchi jirani ya Morocco wanasema.

Ripoti zinasema baadhi ya waliofariki walikuwa wameanguka kutoka juu ya uzio wa mpaka.

Maafisa kadhaa wa usalama na wahamiaji wamelazwa hospitalini kwa matibabu kufuatia makabiliano mapema siku ya Ijumaa.

Ilikuwa ni mara ya kwanza kushuhudiwa kwa majaribio kama haya ya kuvuka kwa wingi tangu Uhispania na Moroko kuanza tena uhusiano wa kidiplomasia mnamo Machi.


Kushuka kwa mahusiano kulikuja baada ya Uhispania kuunga mkono mpango wa kujitawala wa Morocco kwa eneo linalozozaniwa la Sahara Magharibi.

Maafisa wa Uhispania wanasema mamia ya watu walijaribu kupenya ndani ya eneo hilo baada ya kukata uzio.

Wengi walilazimishwa kurudi lakini zaidi ya 100 walifanikiwa na walikuwa wakishughulikiwa katika kituo cha mapokezi, waliongeza.


Melilla na Ceuta, eneo jingine la Uhispania, katika miaka ya hivi karibuni limekuwa kitovu cha wahamiaji wengi kutoka Kusini mwa Jangwa la Sahara wanaojaribu kufika Ulaya.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad