Watuhumiwa wa mauaji ya mtoto Geita wakamatwa



Jeshi la Polisi mkoa wa Geita linawashikilia watu wanne wakazi wa kata ya Ibambila wilayani Nyanghwale kwa tuhuma za kumbaka na kumuua hadharani Dorcas Mathias mtoto wa miaka 7, huku wakihusishwa na imani za kishirikina.
Katika watuhumiwa hao watatu ni wa familia moja na mmoja ni mganga wa kienyeji

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Geita Henry Mwaibambe anasema waliwakamata vijana wawili wa familia moja na mganga wa kienyeji lakini badae waliamua kumkamata mama wa watuhumiwa wawili baaada ya kuitishia familia iliyofiwa kuwa atakufa na mwingine.

Wakizungumzia matukio ya ukatili kwa mkoa wa Geita, mkuu wa wilaya ya Nyanghwale Jamhuri William na zimekuwa zikipokea Rushwa kutoka kwa watuhumiwa hali inayopelekea watuhumiwa kutochukuliwa hatua za kisheria.

Mkuu wa mkoa wa Geita Rosemarry Senyamule amegiza idara inayohusika kusajili waganga wa jadi wilayani humo kuwatambua waganga halali ili kuwaondoa wanapiga ramli chonganishi ili kuondoa vitendo vya mauaji yanayotokana na Imani za kishirikina.

Aidha Jeshi la Polisi mkoani humo limefanikiwa kuwakamata watu watano kwa tuhuma za mauaji ya Nkeya Thomas mtoto wa miaka miwili alieuwawa kwa kukatwa shingo

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad