Waziri Makamba Akanusha Taarifa za Kupanda Kwa Bei ya Umeme "Puuzeni Taarifa Hizo"



Dodoma. Serikali imewataka wananchi kupuuza taarifa za kwamba bei ya umeme imepanda nchini.

Hayo yamesemwa leo Ijumaa Juni 9, 2022 na Waziri wa Nishati, Januari Makamba wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Nyasa (CCM), Stella Manyanya.

Mbunge huyo alihoji kama ni kweli bei ya umeme imepanda maana katika mitandao ya kijamii kuana taariza inazunguka kuwa bei ya umeme imepanda.

Akijibu swali hilo, Makamba amesema si kweli kwamba bei ya umeme imepanda na kuwa Serikali inasikitishwa na uvumi huo.


Amesema kuwa tayari wameshazitaka mamlaka zichukue hatua kwa watu ambao wanaeneza uvumi huo.

“Mchakato wa kupandisha bei za umeme ni mrefu na unahusisha maoni na wadau ni lazima washirikishwe pale bei inapotaka kupandishwa,”amesema Makamba.

Amesema mchakato huo sio wasiri ni lazima uwashirikishe wadau watoe maoni yao.

Naye Mbunge wa Viti Maalum, Salome Makamba alihoji Serikali inampango gani wa kuhakikisha kuwa maeneo ya viwanda katika jimbo la Shinyanga mjini yanapata umeme.

Akijibu swali hilo Makamba amesema Shirika la Umeme nchini (Tanesco) limeanzisha programu kwenye maeneo ya uzalishaji ikiwemo kwenye viwanda na migodi.

Amesema katika programu hiyo itawahusu pia maeneo ya Shinyanga Mjini.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad