Yanga yasimamisha Kariakoo, Simba wajibu




Yanga wamesimamisha Kariakoo hakuna anayepita wala anayefanya manunuzi wakipita na msafara wao na kombe lao la ligi.

Msafara wa Yanga umetinga Kariakoo karibu kabisa na makao makuu ya watani wa jadi Simba kisha mashabiki wao kusimamisha wakiwaringia wenzao.

Yanga wameimba nyimbo zao wakiwaringia Simba wakiwatania kwa jina la utani Makolo makolo makolo.

Hata hivyo Simba nao hawakuwa wanyonge walitoka na baadhi ya makombe yao na kuwatambia wenzao.


 
Mwisho Yanga wakamalizia kwa kuanza kuimba kwa kishindo wakitaja jina la wadhamini wao GSM GSM GSM GSM na kuwanyamazisha wenzao.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad