Yes Rayvanny Kafanya Video ya Gharama Lakini Inapashwa Aambiwe Awekeze Kwenye Technolojia Hata Ulaya Siku Hizi Hawachomi Nyumba Live


Hatimaye lile movie la “I miss You”, la Kwake @rayvanny ft @officialzuchu limetoka huku Rayvanny akidai ametumia muda wa miezi mitatu kulishoot na kutumia pesa nyingi kiasi kwamba inawezakana ikawa ndio video yenye gharama kubwa zaidi kuwahi kutokea hapa Bongo. Jambo kubwa linalofanya Video hii iwe ya gharama zaidi ni muda uliotumika kuishoot, lakini pia msanii huyo amechoma moto nyumba aliyoijenga, kusudi aweke uhalisia kwenye industry ya Tanzania. Swali ni je, vipi kama hiyo scene ingekosewa na kutakiwa kurudiwa au vipande vya video vingecorrupt na tayari nyumba imechomwa,ingekuwaje?


Alicho kifanya Rayvanny kinapaswa kupongezwa 100%, hakijawahi fanywa nchini,lakini cha kumshauri ni kuwa teknolojia inaweza kukupa uhalisia na watu wakaamini kwenye project yako,na ndio huko wasanii na madirector wangepaswa kuwekeza zaidi, Leo hii movies za misituni,za kivita si ajabu ukiambiwa 99% zinachezwa kwenye studio za Marval, na ukiangalia zinakupa uhalisia.


Kabla ya Teknolojia kukua,wenzetu walikuwa wanachoma na kuharibu kweli vitu vyao,ila sometimes inatokea,scene zimeshootiwa, material yanakaguliwa hayasomi,script inahitaji uchome helicopter,utachoma helicopter ngapi? So Teknolojia imeweka suluhu kwenye yote haya,japo ni gharama kubwa. Yote kwa yote, Big up Chui kwa uthubutu.


Maoni ya mdau✍🏻

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad