Young Africans kuanzia hatua ya awali Ligi ya Mabingwa Afrika





Shirikisho la Soka Barani Afrika ‘CAF’ leo Jumatatu (Juni 06) limethibitisha klabu ya Young Africans itaanzia hatau ya awali ya Michuano ya Klabu Bingwa Barani Afrika msimu ujao wa 2022/23. 

CAF imethibitisha uratibu huo, kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii kwa kuweka Video inayoonyesha Mshsamabuliaji wa klabu hiyo Fiston Mayele akiwasalimia mashabiki walipokua njiani. 

Young Africans itashiriki Michuano hiyo, kufuatia kuwa na uhakika wa kutwaa Ubingwa wa Tanzania Bara msimu huu, huku ikibakisha alama tatu kufikia lengo hilo. 

Katika hatua nyingine CAF imesisitiza klabu zote ambazo zitashiriki michuano ya Kimataifa kuhakikisha zinawasilisha mapema orodha ya majina ya wachezaji watakaosajiliwa kwa ajili ya michuano hiyo. 

Msimu uliopita Young Africans ilishiriki Ligi ya Mabingwa Barani Afrika, lakini ilitolewa katika hatua ya awali kwa kufungwa jumla ya mabao 2-0 na Rivers United ya Nigeria. 

Msimu ujao Tanzania itawakilishwa na timu mbili kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika, na mbili nyingine zitashiriki michuanio ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika. 
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad