Young Africans yakabidhiwa Kombe la Ubingwa Ligi Kuu

 


Hatimaye Klabu ya Young Africans leo Jumamosi (Juni 25) imekabidhiwa Kombe la Ubingwa wa Tanzania Bara msimu wa 2021/22 katiak Uwanja wa ugenini.


Young Africans imekabidhiwa Kombe hilo mjini Mbeya, baada ya mchezo wa wake wa Mzunguuko wa 29 dhidi ya Mbeya City FC, uliopigwa Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine.


Young Africans ambayo bado haijapoteza mchezo katika Mshike Mshike wa Ligi Kuu msimu huu, imelazimishwa sare ya bao moja kwa moja dhidi ya Mbeya City, ambayo imefanya hivyo tena baada ya kupata matokeo ya bila kufungana dhidi ya Wananchi, kwenye mpambano wa Mzunguuko wa Kwanza uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.


Hadi inakabidhiwa Kombe la Ubingwa Tanzania Bara leo Jumamosi, Young Africans imefikisha alama 71 zinazoiweka kileleni mwa msimamo, huku Simba SC iliyocheza michezo 28, ikiwa nafasi ya pili kwa kufikisha alama 60.


Hata hivyo Young Africans ilijihakikishia Ubingwa wa Tanzania Bara msimu huu, juma lililopita baada ya kuichapa Coastal Union mabao 3-0, katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.


Young Africans imesaliwa na mchezo mmoja mkononi kukamilisha ratiba ya msimu huu 2021/22, dhidi ya Mtibwa Sugar ambao utaunguruma katikati ya juma lijali, kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.


Wakati Young Africans ikitarajia kumaliza Ligi Kuu msimu huu kwa kucheza na Mtibwa Sugar, Watani zao Simba SC watamaliza msimu ugenini kwa kucheza dhidi ya Mbeya Kwanza FC, kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea mkoani Ruvuma.


Simba SC kesho itacheza mchezo wa 29 kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya dhidi ya Tanzania Prisons, na tayari wameshawasili jijini humo.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad