Aliyemuua Mke Wake Dar Akamatwa

 


Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam limemkamata Selemani Malima Mkazi wa Keko Mwanga kwa tuhuma za mauaji ya mke wake Husna Majaliwa aliyekuwa mkazi wa Goba kwa Awadhi kwa kumchoma na kitu chenye ncha kali tumboni


.Tukio hilo lilitokea tarehe 12/06/2022 huko maeneo ya Goba, Kinondoni na mara baada ya tukio hilo alitoweka.


Taarifa ya polisi imeleza kuwa Uchunguzi wa awali unaonesha kulikuwa na mgogoro wakifamilia baina ya wawili hao.


Inaelezwa kuwa mtuhumiwa huyo  alifika nyumbani kwa wazazi wa marehemu kumsalimia mzazi mwezake pamoja na mtoto, wakati wakiwa katika maongezi ndipo mtuhumiwa alimshambulia kwa kisu mke wake na kumsabishia kifo.


Mtuhumiwa ameonesha kisu alichotumia kumuua mke wake

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad