Amber Lulu Anasa Kwenye Penzi Zito la Kiben Ten

 


LULU Euggen almaarufu Amber Lulu ; ni mwanamama mwenye kipaji kikubwa kunako Bongo Fleva ambaye uzalendo wa kuishi singo umemshinda na hatimaye amenasa kwa kijana mdogo (kibenteni) anayefanya poa kwenye Bongo Fleva aitwaye The Dream ambaye anatajwa kuwa mpenzi wake mpya.

Amber Lulu ameachia picha ya kimahaba akiwa na The Dream na kunogesha tetesi za kuwa kwa sasa anajipumzisha kwa msanii huyo ambaye kwa muonekano ni mdogo kiumri zaidi yake.

The Dream ni msanii wa Bongo Fleva anayechipukia kwa kasi ya kipekee kwenye tasnia hiyo tangu alipoachia wimbo wake wa kwanza uitwao Hola mwishoni mwa mwaka jana.

Msanii huyo aliesainiwa chini ya Lebo ya Katemi Empire yenye makazi yake jijini Tanga kwa sasa anamiliki mkwaju wa I Love You ambao wengi wanaamini amemuimbia Amber Lulu.

Gazeti la IJUMAA lilimtafuta meneja wa The Dream, Jr Junior ili kujua ukweli wa penzi hilo baada ya jitihada za kumpata Amber Lulu na The Dream kuwa na ugumu kidogo, alisema; “Kwani kuna ubaya wa The Dream kuwa na mtoto mkali?

“By the way suala la mahusiano linabaki kuwa binafsi yake au ni ishu yao wawili mimi natazama zaidi kwa upande wa kazi zake. Hizo picha na tetesi nimeona na kusikia kama Mtanzania mwingine alivyoona au

@iamamberlulu

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad