Auawa kwa Kukatwa na Bawa la Helikopta, Ndugu yake Ashuhudia Tukio Zima




Eneo la tukio alipofariki kijana mwenye umri wa miaka 21 mtalii kutoka nchini Uingereza
MTALII kijana raia wa Uingereza mwenye umri wa miaka 21 amefariki baada ya kukatwa na bawa la helikopita mbele ya ndugu yake wakati wakitua kutoka katika mji wa Athens wakitokea katika mji wa Mykonos nchini Ugiriki walikoenda kwa ajili ya Utalii.

Taarifa zinadai baada ya kushuka alitembea nyuma ya mkia wa Helikopta huku injini ikiwa inaendelea kufanya kazi ndipo alipocharangwa vipande vipande huku ndugu yake akishuhudia tukio zima.

Ajali hiyo imetokea majira ya saa 12:20 jioni ambapo mara moja gari la huduma kwa wagonjwa lilifika mara moja kwenye Helikopta ambayo ilikuwa ni usafiri binafsi wa familia hiyo ya kitajiri.


Kijana huyo alifariki kwa kucharangwa na bawa la Helikopta
Tayari Rubani wa Helikopta hiyo ameshatiwa mbaroni huku waongoza ndege wa zamu nao wakitiwa nguvuni pia kwa ajili ya kupisha uchunguzi wa tukio hilo.


 
Kwa mujibu wa taarifa ya awali ya Polisi ni kwamba propela huzunguka kwa muda wa dakika 2 ikiwa ni baada ya Helikopta kutua au kubonyeza kitufe cha kuzima ndani ya sekunde 50 mara baada ya Helkopita kutua.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad