Baba Levo Amuonya Rayvanny, Asibadilike na Kuwa kama Harmonize




Baba Levo amemshauri Rayvanny kuendelea kumheshimu Diamond Platnumz

BABA Levo au Chawa Promax wa Diamond Platnumz; ni msanii na mtangazaji wa Wasafi ambaye hajabaki nyuma kuzungumzia suala la msanii Rayvanny kuondoka Lebo ya WCB Wasafi na kuanzisha yake binafsi ya Next Level Music (NLM).

 

Baba Levo amemuonya Rayvanny dhidi ya kuondoka kisha kuanza kumsema vibaya Diamond kama ambavyo walifanya watangulizi wake, Harmonize na Rich Mavoko.

 

Baba Levo anasema endapo Rayvanny atakiuka maneno hayo basi awe tayari kwa vita vya moto maana yeye siku zote ni mpambanaji aliyejiandaa kivita, iwe ya maneno au ya kurushiana mikwara na masumbwi.


Baba Levo amemshukuru Rayvanny kwa kumsaidia kumpelekea kwa Diamond Platnumz

Anasema kwamba, Rayvanny ndiye aliyemleta katika familia ya WCB Wasafi na sasa ameondoka na kumuacha na kumtakia kila la kheri katika safari yake mpya kimuziki.

 

“Kwa heri ndugu yangu Rayvanny, ulinileta Wasafi umeniacha. Mungu akusimamie kwenye kila jambo. Hakikisha husahau heshima uliyojengewa na Diamond. Yeye ndiye chanzo cha mabadiliko yetu kwenye maisha yetu ya muziki,” kwa mara ya kwanza Baba Levo anaonekana kutoa ushauri uliotukuka.

 

Jana Julai 12, 2022, Rayvanny alitangaza kuondoka rasmi kwenye Lebo ya Wasafi na kumsifia pakubwa msanii Diamond kwa kumpa nafasi ya kuonesha kipaji chake kwa dunia.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad