Babu Tale amjibu P Funk Majani kuhusu Wasafi kuwanyonya wasanii

 


“Kama mkongwe kasema si vizuri kubishana naye, acha aseme, namuheshimu sana P Funk, mwache. Mikataba ya WCB haipo kwenye maiki ama kamera. Ulishawahi kumuona mtu amebandika mikataba kwenye kamera au maiki? Heshima ya Majani kwenye hii industry ya muziki ni kubwa, basi tumwache" Babu Tale aliwaambia waandishi wa habari waliomuuliza na kuendelea


“La ndani linabakia ndani, ukimwona mtu analitoa la ndani kuwa la nje hajafundwa huyo. Nina miaka mingi kwenye industry ya muziki, nazungumza ninachoikifahamu, lakini tunabadilisha kutoka kwenye muziki wa kawaida kuwa biashara.


“Lazima kuwe na mikataba na makubalianao na makubaliano ni ya ndani, unapoona mtu anasimama kuyachambua makubalianao, ana mashaka. Na ukiona mtu anachambua mkataba wa pande mbili ambao hahusiki kwa namna yoyote achana naye, muheshimu.


“Kuhusu Rayvanny, Harmonize, Mavoko kujitoa sisi hatuna la kusema, sisi ni wafanyabiashara kwa hiyo tunaruhusu mtu yeyote aseme anachoona. Afrika nzima inatambua mchango wa WCB.


“Usiwaache watu wakutoe kwenye reli yako, vision yetu ni kutoka kimataifa, ukiwaacha watu wakutoe kwenye reli halafu ukawafuata, unatoka kwenye kile ambacho umekidhamiria, hatuko tayari.


“Hatuwezi kuvunjika moyo, sisi ni wafanyabiashara wa muziki na muziki unatulipa kwelikweli, hatuoni sababu ya kuacha. Unapofanya biashara inayolipa lazima kuwe na makelele.


“Ukimuona mtu anapiga kelele kwenye biashara ya mtu anayopiga pesa, ujue yeye kuna sehemu ana matatizo, usibishane naye, mheshimu. Ukiona mtu anabishana na na sisi mpe big-up,” amesema Tale amewaambia waandishi wa habari

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad