Basi la Shule Lapata Ajali na Kusababisha Vifo vya Watu 10, Rais Atuma Salamu za Pole



BREAKING: Rais Samia Suluhu Hassan, ametuma salamu za pole kufuatia basi la wanafunzi wa Shule ya King David Mtwara lenye namba za usajili T 207 CTS lililopata ajali asubuhi ya leo Jumanne, Julai 26, 2022 eneo la Mikindani Mtwara likiwa na wanafunzi na kuua watu 10 wakiwemo wanafunzi nane wa shule hiyo.



Kupitia akaunti yake ya Twitter, Rais Samia ameandika: “Nimesikitishwa na vifo vya wanafunzi 8 wa Shule ya Msingi ya King David na watu wazima 2 vilivyotokea leo asubuhi huko Mtwara Mikindani baada ya gari la shule kutumbukia shimoni. Nawapa pole wafiwa, mkuu wa mkoa na jamaa. Mwenyezi Mungu awarehemu marehemu na kuwaponya majeruhi.



Taarifa zaidi kuhusu ajali hiyo zitakujia hivi punde.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad