Klabu ya soka ya Yanga imethibitisha kumsajili mshambuliaji raia wa Ghana Benard Morison.
Mshambuliaji huyo machachari amesajiliwa na klabu ya Yanga akitokea katika klabu ya Simba Sports alikoitumikia Kwa misimu kadhaa.
Hivi karibuni klabu ya Simba ilitoa taarifa Kwa uma ikieleza kuwa imempa likizo mshambuliaji huyo kwa ajili ya kutatua matatizo ya kifamilia yaliyokuwa yanamkabili huko nchini kwao.
Hatahivyo usajili huo baadhi ya mashabiki na wapenzi wa klabu ya Yanga wameinesha wasiwasi kutokana na tabia za mara Kwa mara za utovu wa nidhamu Kwa mchezaji huyo.
Je! Unafikiri klabu ya Yanga imefanya sahihi au itakuwa imerejea ilikotoka Kwa kumsajili mchezaji huyo, weka comment yako hapo chini juu ya usajili huo.