BREAKING: Msuva Ashinda Kesho FIFA..Kulipwa Bilioni 1.6


BREAKING: Shirikisho la Soka Duniani FIFA limeiagiza Club ya soka ya Wydad Casablanca ya Morocco kumlipa Mchezaji Mtanzania Simon Msuva @smsuva27 zaidi ya dola za kimarekani laki saba ( Tsh. zaidi ya bilioni 1.6) baada ya Mchezaji huyo kushinda kesi ya madai aliyoifungua dhidi ya Club hiyo.

Msuva ambaye alikua amesaini mkataba wa miaka minne alilazimika kuusitisha mkataba wake December mwaka 2021 kutokana na kuidai Club hiyo malimbikizo ya mishahara pamoja na pesa za usajili (signing fee).

Taarifa EXCLUSIVE zilizoifikia millardayo.com na AyoTV usiku huu zimeeleza kuwa hukumu ya FIFA imeamuru Mchezaji huyu alipwe na riba pia.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad