Breaking News: Rais Samia Atengua Uteuzi wa Mkurugenzi wa Bandari (TPA)



Eric Hamissi, aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA)

RAIS Samia Suluhu Hassan ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Eric Hamissi.

Taarifa iliyotolewa leo na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus imeeleza kuwa nafasi ya Hamissi, itachukuliwa na Plasduce Mkeli Mbossa ambaye uteuzi wake unaanza leo, Julai 4, 2022.

Kabla ya uteuzi huo, Mbossa alikuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania.

Hamissi ameondolewa kwenye wadhifa huo, baada ya kuhudumu kwa takribani mwaka mmoja na miezi mitatu, ambapo aliteuliwa na Rais Samia April 4, 2021 kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) akichukua nafasi ya Eng. Deusdedith Kakoko.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad