China yatoa onyo kali kwa Marekani




Wizara ya Mambo ya Nje ya China imetoa onyo zito kwa Spika wa Marekani Nancy Pelosi ambaye yuko katika ziara rasmi nchini Taiwan.

Taarifa ya wizara hiyo iliyochapishwa katika gazeti la Financial Times ilisema ‘’Beijing yatoa onyo kali zaidi kwa Washington.

China imesema iwapo Marekani haitazingatia onyo hilo itachukua hatua kali japo haikusema kuwa hatua hiyo ni ya kijeshi.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Zhao Lijian alisema Washington inataka kufafanua msimamo wake kuhusu Taiwan.

Ikulu ya White House ilikataa kujibu maoni ya Uchina.

Serikali ya Taiwan ilisema kwamba mustakabali wa kisiwa hicho utaamuliwa na watu milioni 23 wanaoishi katika kisiwa hicho

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad