Kama wewe ni mwanaume utajuwaje huna uwezo wa kumpa mwanamke ujauzito!?
Kama na wewe ni mwanamke utajuwaje mmeo ni mgumba kwamba hana uwezo wa kukupa ujauzito?
Namna rahisi kabisa ya kufahamu hilo ingekuwa ni kufanya vipimo.
Kwa kawaida mbegu za mwanaume zingechukuliwa na kufanyiwa vipimo na uchunguzi zaidi (sperm analysis) na daktari angetoa majibu ikiwa mwanaume husika ni mgumba.
Bila vipimo hakuna namna rahisi ya kuhitimisha kwamba mwanaume husika ni mgumba au hana uwezo na afya ya kuweza kumpa ujauzito mwanamke.
Hata hivyo kuna dalili kadhaa zikijitokeza tunaweza kuanza kuwa na wasiwasi huenda mwanaume husika ni mgumba au ana tatizo fulani la kiafya linalomzuia kutungisha ujauzito.
Kuna wanaume siyo wagumba bali wana tatizo fulani ambalo likiwekwa sawa hilo basi ataweza kumpa tena ujauzito mwanamke bila shida yoyote.
Huenda mwanaume huyo amepatwa na changamoto ya mbegu zake kuwa chache, labda hazina afya nzuri au hazipo tu sawa.
Kwahiyo pamoja na hizi dalili ninazotaka kukueleza hapa bado nakushauri usitumie dalili hizo kufanya hitimisho lolote juu ya afya yako au ya mmeo juu ya uwezo wake wa kutungisha mimba.
Dalili za mwanaume mgumba ;
1. Mke kushindwa kushika ujauzito
Dalili ya kwanza kubwa kabisa kuliko zote zitakazokuonyesha huenda mwanaume ni mgumba ni kitendo cha mkewe kutoshika ujauzito.
Kama ameshaoa na anaishi na mke na muda mrefu umepita labda miaka miwili au hata zaidi basi hii ndiyo dalili ya kwanza.
Ingawa kwenye familia nyingi wa kwanza kupima atakuwa ni mwanamke!
Lakini inapotokea mwaka mzima au miaka miwili au zaidi inapita na hakuna dalili yoyote ya ujauzito ni ishara huenda mme ana tatizo la uzazi.
Hii ndiyo sababu huwa nawashauri wanawake wengi wanaohangaika na matatizo ya uzazi kuwahimiza na waume zao nao wafanye vipimo.
Mara nyingi nimesema kwamba hakuna sababu au ulazima wa wanandoa kupata ujauzito au mtoto ndani ya mwaka mmoja tangu waanze kuishi pamoja.
2. Matatizo fulani kuhusu ufanisi na uwezo wa kuhimili tendo la ndoa
Kama mwanaume ana udhaifu fulani au uwezo mdogo katika kushiriki na kumudu tendo la ndoa ni ishara inayoweza kuonyesha uwezo wake mdogo katika kutungisha mimba pia.
Mfano kama mwanaume ana hisia ndogo sana au hana hisia ya kutaka kushiriki tendo la ndoa mara kwa mara inaweza kuwa ni dalili mojawapo ni mgumba au hana uwezo wa kutungisha mimba.
Kama mwanaume ana uwezo mdogo sana wa kusimamisha uume wake, kama uume wake siyo mgumu yaani upo lege lege tu na unaweza kusinyaa muda wowote basi nayo yaweza kuwa ni dalili za mwanaume mgumba.
3. Kumwaga mbegu chache sana na nyepesi.
Mwanaume mwenye afya nzuri ya Uzazi bao lake la kwanza kawaida huwa na ujazo mwingi na nzito nzito siyo nyepesi.
Kama bao la kwanza tu linaloonekana ni vimajimaji tu vichache na vyepesi tu na pengine hajashiriki tendo la ndoa siku 3 au zaidi basi hii dalili kwamba hana uwezo wa kutungisha ujauzito.
Kama mwanaume anatoa mbegu chini ya milioni 39 kwa bao moja ni wazi atapata tabu sana kwenye kutungisha ujauzito.
4. Ana dalili fulani za homoni zake kutokuwa sawa.
Kama ilivyo kwa mwanamke, mwanaume pia ili awe na uwezo wa kutungisha ujauzito lazima homoni zake mhimu hasa zinazohusiana na uzazi ziwe sawa na zinapatikana.
Dalili kuu ya mwanaume ambaye homoni zake huenda zimevurugika ni pamoja na mwanaume husika kuota matiti makubwa yanayokaribia kama ya binti mdogo tofauti yalivyo ya mwanaume wa kawaida.
Dalili nyingine ni pamoja na kuwa na hasira nyingi bila sababu, kupenda kujitenga na watu na msongo wa mawazo wa mara kwa mara.
Dalili zingine ndogo ndogo ni pamoja na ;
5. Uvimbe kwenye korodani
6. Kupoteza uwezo wa kunusa harufu
7. Maumivu ya mara kwa mara kwenye korodani.
8. Kuwa mdhaifu kwa ugonjwa wa kisukari
9. Upungufu sugu wa nguvu za kiume
Kama nilivyosema pale mwanzo kwamba hizi ni dalili tu, vipimo zaidi vitahitajika ili kupata hitimisho.
Ikiwa wewe ni mwanaume na umekuwa ukitafuta dawa ya asili kwa ajili ya kukusaidia kutungisha mimba niachie tu ujumbe WhatsApp +255714800175