Watu 17 wameteuliwa kutunzwa medali za heshima na Rais wa Marekani, Joe Biden na mwigizaji nguli Denzel Washington ni mmoja wao.
Orodha ya Rais Biden ya watu ambao amewachagua kuwatunza inajumuisha walio hai na walio aga dunia kutoka nyanja mbali mbali kama vile michezo, uigizaji, siasa, ulinzi, masomo na utetezi wa haki.
Rais Biden atawavisha medali hizo siku ya Alhamisi wiki hii, Julai 7 kwenye Ikulu ya Whitehouse nchini Marekani, huku Denzel Washington akiwa ndiye mwigizaji pekee aliyeteuliwa mwaka huu katika sekta ya filamu.
Fahamu, tuzo hizo hutolewa kila mwaka mwezi wa saba wakati wa kuadhimisha siku nchi hiyo ya Marekani ilijipatia uhuru wake.