Diamond Platnumz Kumuharibu Zuchu Aisee......Kaiga Hili..


Zuchu; ni msanii wa moto ile mbaya kunako lebo kubwa kabisa kwenye ukanda wa Afrika Mashariki ya Wasafi Classic Baby (WCB) ambaye anazidi kuwa gumzo kutokana na tetesi za mahusiano baina yake na bosi wake, Diamond Platnumz ambaye anadaiwa kumharibu mrembo huyo.

Diamond anadaiwa kumfundisha Zuchu maisha ya kufeki baada ya mrembo huyo kuposti zake akiwa amemuiga katika mitindo yake.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Zuchu ameposti picha na video akionesha jinsi ambavyo amemuiga Diamond kwa kuweka urembo katika meno yake pamoja na pete za kimapambo; pete moja kubwa kwenye kidole cha mwisho cha mkono wa kulia, kama ambavyo Diamond anavaa.

Akiwa nchini Afrika Kusini akiandaa video mpya, Zuchu amezua gumzo kama lote kutokana na uigaji huo kwa bosi wake na kufanya wengi waamini kwamba wawili hao wapo kwenye mahusiano; uvumi ambao umekuwa ukizungumziwa zaidi kwa muda mrefu sasa.

“Hapa sasa ni tabasamu zuri tu. Ahsante sana Diamond Platnumz,” anasema Zuchu akifuatisha na picha hizo na maneno hayo yaliyoonekana kwamba anamshukuru bosi wake kwa kumfunza mbinu hizo za kujiremba ambazo kwa muda mrefu zimekuwa ni za Diamond tu mpaka kuwa kama nembo ya utambulisho wake.

Sasa, waja kama kawaida yao, wamezuka kwenye picha hizo alizozipakia Zuchu na kuachia yao ya moyoni ambapo walisema sasa huo ni uthibitisho tosha kwamba wawili hao wamepanga kuigana hadi uvaaji maana wao ni mwili mmoja kimtindo.

Zuchu na Diamond kwa muda mrefu wamekuwa wakisemwa kuwa wapo katika mahusiano japokuwa hakuna hata mmoja baina yao amekiri wazi wala kukataa bayana uwepo wa mahusiano yao.

Zuchu amekuwa akibanwa sana katika mahojiano kwa maswali ya uwepo wa mahusiano yao, lakini amekuwa akiguna na kumalizia kwamba anamchukulia Diamond kama bosi wake kimuziki.

Kwa upande wake, Diamond amekuwa akiulizwa ambapo wakati mmoja wakiwa kwenye mahojiano na pamoja na Zuchu, mwanadada huyo aliulizwa swali la kuchumbiana na Diamond, lakini Simba akadakia kwa haraka na kumkatiza huku akisema kwamba maswali kama hayo yana ukakasi na ndiyo maana alimsaidia Zuchu kujibu ili asije akazungumza mambo yasiyofaa.

Familia nzima ya WCB imekuwa ikilikwepa suala hilo

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad