Dimpoz Afukua Makaburi Kuwekewa Sumu Afe, Amtaja Mama Yake Mzazi


OMMY Dimpoz; ni staa wa muziki wa Bongo Fleva ambaye amefukua makaburi juu ya ile ishu yake ya kuwekewa sumu nusura apoteze uhai.

Baada ya tukio hilo lilitokea mwaka 2018, Dimpoz alibaki akipambania uhai wake huku akifanyiwa oparesheni tatu maalum za koo katika juhudi za kuokoa maisha yake.

Juzi wakati akitumbuiza katika Kipindi cha Break Point, Dimpoz alisikika akiimab; “Sumu waliniwekea, bado nusu nikufuate mama…”


Hii inatafsiriwa kwamba kwa sasa angekuwa marehemu, kwani ilibaki kidogo amfuate mama yake ambaye ametangulia mbele za haki.

Ommy Dimpoz amesema aliwekewa sumu

Dimpoz ambaye ameuanza vyema mwaka huu huku tayari akiwa ameachia ngoma mbili, aliwahi kufichua kuwa tatizo la koo lake lilitokana na sumu.

Dimpoz alisema kuwa, sauti yake ilirudi kabla ya kupelekwa nchini Ujerumani ambako alifanyiwa oparesheni ya tatu na ya mwisho.

Cc; @sifaelpaul

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad