Dimpoz Akiri Kuwekewa SUMU "Nusu Nikufuate"


Mwimbaji nyota wa muziki nchini, msanii @ommydimpoz amekiri mbele ya mashabiki kuwahi kuwekewa sumu ili afe, katika tukio lilitokea mwaka 2018 lililomfanya akafanyiwa oparesheni tatu kubwa ya koo lake akipambania kuokoa maisha yake.


Akiwa na mwimbaji Christian Bella jana Jumapili, ndani ya 'Break Point' Makumbusho, waliitumbiza pamoja kolabo yao "Nani Kama Mama" ambapo kwenye verse yake @ommydimpoz alisikika akisema, "Sumu Waliniwekea, Bado Nusu Nikufuate Mama" akiwa na maana kwasasa angekuwa marehemu, kwani ilibaki kidogo amfuate mama yake ambaye ameshatangulia mbele za haki.


@ommydimpoz ambaye ameuanza vyema mwaka huu akiwa tayari ameachia ngoma mbili, aliwahi kusema athari ya koo lake ni matokeo ya sumu. Na kwenye interview yake na Millard, Ommy alisimulia sauti yake ilivyorudi, ni kabla hajapelekwa Ujerumani alikofanyiwa oparesheni ya tatu ambayo ilikuwa ya mwisho.


Ikumbukwe, ni takribani miaka mitatu sasa imepita Dimpoz hakuonekana jukwaani akitumbuiza. Hata hivyo hii inakuwa mara yake ya pili baada ya Machi 20 mwaka huu, kutumbuiza kwenye tamasha lake aliloliita "Cheusi Cheupe" lililofanyika katika viwanja vya Zakhem, Mbagala jijini Dar es salaam.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad