Eric Omondi: Mimi si shoga, kama hamuamini basi leta 'madem' wenu kwangu



Mchekeshaji Eric Omondi ameweka wazi kuhusu madai ambayo yamekuwa yakimuandama kwamba yeye ni wa kile chama cha ushoga kutokana na ‘skits’ zake za mitandaoni ambazo anacheza akiwa amevalia kike na kuigiza kama mwanamke kwa jina Diva.

Akizungumza na Eve Mungai, Omondi amekanusha kwamba yeye si shoga na kusema ile ni maisha ya kuigiza tu na watu wanafaa kutofautisha maisha ya mitandaoni na maisha ya uhalisia.


Alisema kwamba igizo hilo analoigiza kama Divalacious ni mtu fulani tu ambaye alijengeka kimaudhui wakati wa virusi vya Corona ambapo serikali ilikuwa imeweka kafyu.

Msanii huyo alisema kwamba wafuasi na mashabiki wake wengi ni wa jinsia ya kike ambao wanachukua asilimia 72, asilimia iliyosalia ikiwa ni ya wanaume.

“Kila muda nikifanya maigizo yangu lazima nifanye kitu ambacho kinavutia kwa wanawake. Kitu ambacho watakaa wakumbuke kwamba enyewe, kama Diva anajaribu kuigiza kama mwakamke kwa sababu Churchill aliniambia ukifurahisha wanawake umefurahisha kila mtu,” Omondi alitetea igizo lake hilo la kuvalia kama mwanamke na kujipodoa.

Muigizaji huyo pia alisema pindi tu anapovalia nguo za kike basi sauti yenyewe ya kuigiza kama Diva huja yenyewe hata bila kulazimisha.

Omondi alisema si leo ameanza kuvalia hivyo kwani alipoanza mwaka wa 2008 alianza kuvalia hivo na watu ni muda sasa wamzoee.

Akitilia mkazo kwamba yeye si shoga, Omondi aliwataka wale wanaotilia shaka kwamba yeye ni shoga basi wampelekee wapenzi wao wa kike na wasubiri matokeo kama kweli yeye ni wa mrengo wa kushoto ama kulia.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad