Mange Amshukia Diva "Eti ntakuwa chini yako ntaishi kwa misingi yako, ni Upuuzi"



"Eti ntakuwa chini yako ntaishi kwa misingi yako. wanawake tunalilia equality na wanaume eti mtu naandika upuuzi kama huu" - Mange Kimambi

"Eti ntakuwa chini yako ntaishi kwa misingi yako. wanawake tunalilia equality na wanaume eti mtu naandika upuuzi kama huu" - Mange Kimambi


Mkuza maudhui wa muda mrefu Mange Kimambi amelivalia njuga Sakata la kuvurugika kwa ndoa ya mtangazaji wa Wasafi FM Diva thee Bawse na mumewe wa ndoa sheikh Abdulrazak Salum.

Kupitia kwenye App yake, Kimambi amemfuma Diva thee Bawse kwa kutumia mkuki wake mwenyewe kwa maana ya kumshambulia kwa kutumia maneno yake aliyoyaandika Instagram kumtaka samahani mumewe Salum.


 
Mange Kimambi alimfanyia utani Diva kwa kumwambia kwamba msamaha wake kwa Salum umekubalika ila kwa sharti kwamba lazima akubali mshahara wake wote anaoupata pale Wasafi kuingia kwenye akaunti yake ili yeye afanye mipango ya kila kitu kama mume wa nyumba.

“@divatheebawse nimeongea na mganga wako. Amekubali kurudi ila kasema ana sharti moja tu, kwavile umekubali kuishi kwa misingi yake na kuwa chini yake kuanzia sasa mshahara wako utakuwa unaingia kwenye akaunti ya benki yake alafu yeye ndo matokeo ya pocket money. Uko tayari? Kama uko tayari sema hata usiku huu anarudi…. Yani mshahara wako kila mwezi lazma umkabidhi yeye then yeye ndo atapanga matumizi maana ushasema yeye atakuwa juu yako na utaishi kwa amri zake.Sema kama uko tayari turudishe majeshi…” aliandika Mange Kimambi.

Mkuza Maudhui huyo ambaye kwa muda mrefu pia amejiongeza kama mwanaharakati wa kukosoa baadhi ya mambo nchini mwake akiwa huko Marekani alizidi kusema kutupa vijembe kwa Diva na wanawake wenye fikira kama zake za kumuambia mwanaume kwamba watakuwa chini yake na kulitaja suala hilo kama upuuzi.


“Ila utani pembeni huu ni msiba, kweli in 2022 ambapo wanawake tunalilia equality na wanaume eti mtu naandika upuuzi kama huu kwa mwanaume tena publicly, eti ntakuwa chini yako ntaishi kwa misingi yako? Hata wazazi wetu tuligoma kuwatii kiasi hiki, leo unamsujudia hivi kiumbe ulimjua uzeeni tena ambae wewe ndo unamlisha ili tu uonekane na wewe una mume? Hivi kuna tunzo zinatolewa kwa wanawake wenye ndoa? Badala kutumia platform yake ku empower wanawake anatumia jukwaa lake kufundisha wanawake upuuzi huu? Kweli huu ni msiba...” aliendelea kufoka Mange Kimambi.

Kimambi pia alizidi kuwaelezea wanawake kwamba ndoa sio mwisho wa maisha na wala si kila mtu ameandikiwa ndoa kwani ni wakati sasa shinikizo la kutaka ndoa liwatoke na kukubali kwamba ndoa si kigezo katika kufaulu maishani.

udakuspecially.com


CHADEMA yaondoa kortini mapingamizi dhidi kina Mdee


12
ippmedia.com


Habari mpya
Msuva: Rais wa Timu Alikuwa Hapokei Simu Zangu, Nilimuombea Afe


5
1h
globalpublishers.co.tz


Simba yakwea pipa kwenda Misri

6h
spotileo.co.tz


Raila aingilia majibizano ya Ruto, Wamalwa

1h
taifaleo.nation.co.ke


Waonya matumizi holela sare za Jeshi

7h
ippmedia.com


American Used Cars might be shipping to Dar Es Salaam soon (see options)
American Used Cars | Search
The Cost of A Hair Transplant May Surprise You
Hair Transplant | Search Ad
by TaboolaSponsored Links

24

12

10


Tujadili swala hili

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad