Gharama kupima DNA Sh100,000




Mkemia Mkuu wa Serikali, Dk Fidelice Mafumiko
Dar es Salaam. Mkemia Mkuu wa Serikali, Dk Fidelice Mafumiko amesema kuwa anayetaka kupima vinasaba (DNA), iwapo ana wasiwasi na mtoto anapaswa kufuata taratibu, badala ya kwenda moja kwa moja kwenye ofisi ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA).

Akizungumza na waandishi wa habari katika maonyesho ya 46 ya biashara Sabasaba, Dk Mafumiko alisema kuna hatua nyingi za kufuata ili kupata huduma hiyo ikiwamo kutoa taarifa kwa ofisa maendeleo ya jamii na wao ndiyo watapeleka maombi yao GCLA.

“Tukipata maombi kutoka katika mamlaka husika, tunayafanyia kazi. Gharama za kupima DNA ni rahisi sana kwa mtu mmoja ni Sh100,000” alisema Dk Mafumiko.

Mbali na hilo Mafumiko pia alitoa rai kwa wamiliki wa viwanda nchini kutotumia kemikali zenye madhara kwa afya za binadamu.

Alisema kama kauli mbiu inavyosema Tanzania ni pahali salama kwa kuwekeza, hivyo wenye viwanda, wafanyabiashara wanatakiwa kutumia kemikali sahihi bila kuleta madhara kwa watumiaji.

Alisema”Kemikali ina faida viwandani, lakini ikitumika vibaya ina madhara kwa binadamu.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad