Hakimu Agoma Kujitoa Kesi ya Mfalme Zumaridi Mwanza


HAKIMU Mkazi, Monica Ndyekobora wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mwanza, amekataa kujitoa katika kesi ya Mchungaji Diana Bundala, maarufu kama Mfalme Zumaridi kama walivyooomba mawakili wake.

Mapema mwezi huu, jopo la mawakili wa utetezi, likiongozwa na Steven Kitare, liliwasilisha kusudio lao la kumkataa hakimu huyo ingawa hawakutaja sababu za msingi kutaka kufanya hivyo.

Kesi hiyo namba 10 ambayo imeendelea kuzua mjadala katika mikoa ya Kanda ya Ziwa, jana iliendelea katika mahakama hiyo na kuvuta umati wa watu.

Jana, kesi hiyo ilifanyika ili kutolewa uamuzi mdogo wa ombi la mawakili wa utetezi la kumtaka hakimu ajitoe kutokana na kutokuwa na imani naye.

Katika uamuzi huo mdogo, Hakimu Ndyekobora aliwaambia mawakili hao kwamba hawezi kujitoa katika kesi hiyo kwa sababu hakuna sababu za msingi za kisheria.


Baada ya uamuzi huo, Wakili Kitare alisimama na kuomba kesi hiyo isiendelee kwa shahidi kuendelea kutoa ushahidi kutokana na kasoro za matakwa ya kisheria. Kesi hiyo iliahirishwa jana huku upande wa utetezi ukipanga kuwasilisha mahakamani hoja zao kwa kuwa awali waliziwasilisha ofisini kwa hakimu.

Katika kesi hiyo, Zumaridi na wenzake wanane wanakabiliwa na shtaka la kufamya fujo na kuzuia askari polisi pamoja ofisa ustawi wa jamii kufanya kazi yao.

Kesi hiyo iliahirishwa hadi Agosti 10, mwaka huu, itakapoendelea kwa wakili wa utetezi kuwasilisha hoja zao za kumkataa hakimu huyo mbele ya mahakama.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad