Hassan Bumbuli Afunguka "Kombe la Azam Lipo Imara Lililegea Tu Kidogo"


Afisa Habari wa Yanga SC, Hassan Bumbuli, ameeleza kuwa skruu ya Kombe la ASFC ilikuwa imelegea kutokana na kushikwa na watu wengi.


Bumbuli ameeleza hayo leo, wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, mara baada ya kusambaa kwa video ikionyesha Kombe la Azam Sports Federation kama limevunjika.


"Kilichotokea ambacho kinasambaa na watu wanakisambaza mtandaoni lile Kombe huwa kuna wakati linasafishwa huwezi ukaliweka likakaa vile.


"Kuna wakati limepigwa vumbi linatakiwa lisafishwe kwahiyo wanaweka skruu kwa ajili ya kulifungua hiki mnakisafisha peke yake, kile pake yake mnakirudishia.


"Kwasababu sisi ni wengi huyu kalishika yule kalishika skruu ikawa imelegea.


"Lakini kombe lipo liko imara zuri.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad