Msemaji wa mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Haji Manara, amekubali kuomba msamaha kwa Rais wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF), Wallace Karia.
Manara amedai kwake kuomba radhi ni kitu cha kiungwana na sio ushamba kama wengine wanavyodhani.
Hata hivyo amesema, yupo tayari kwa lolote kutoka kwenye mamlaka husika, lakini kitu cha msingi kilikuwa na kuomba radhi kwa kiongozi wa soka la nchi.