Hukumu ya Mwizi Nguli Mtandaoni Hushpuppi Yasogezwa Mbele


Mahakama kuu huko California nchini Marekani imeahirisha tena hukumu ya mwizi nguli mitandaoni ambaye ni raia wa Nigeria, Ramon Abbas (39), maarufu Hushpuppi na badala yake imeisogeza mbele hadi Septemba 21, mwaka huu.


Hapo mwanzo hukumu ya mwalifu huyo wa mitandao ilipaswa kusomwa Februari 14 mwaka huu, lakini Jaji Otis Wright anaeiendesha kesi hii akaisogeza mbele hadi Julai 11, na sasa ameisogeza tena mpaka mwezi Septemba.


Hushpuppi, mwezi Aprili mwaka 2021 alikutwa na hatia kuhusika na makosa ya utapeli na wizi wa mabilioni ya fedha kwa njia ya mtandao pamoja na kukutwa na uthibitisho wa njama za kutaka kufanya wizi kwa njia ya mtandao kwenye shule na klabu ya mpira wa miguu inayoshiriki Ligi kuu ya Uingereza.


Kwa makosa aliyokutwa nayo Hushpuppi ilitajwa kuwa huenda kifungo chake kisiwe chini ya miaka 20.


Ikumbukwe, Hushpuppi alitiwa nguvuni tangu mwezi Juni mwaka 2020 alipokamatwa huko Dubai na kuhamishiwa nchini Marekani ambako mpaka sasa yupo kizuizini akisubiri hukumu yake.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad