Mwanamuziki mahiri kutoka Konde music world wide Ibraah kwa mara ya kwanza amezungumzia tukio la kuvunjiwa nazi nyumbani kwake.
Ibraah amebainsha hayo kupitia mahojiano maalum na Dar24 na kusema kuwa watu wengi wanamshauri kwenda kwa wanganga.
Amesema aliwahi kukuta nazi nyumbani kwake na hakuwahi kujua waliofanya hayo ni nani na leongo lao ni lipi.
“Ushauri unakuwaga ni mwingi sana kwa sababu ya vitu ambavyo vinaendelea wakati mwingine, kwa mfano kama kuna siku niliamka nikakuta wamevunja nazi nyumbani kwangu,” alisema Ibraah.
“Sijawahi kuamini sana kuhusu hivyo vitu kwasababu, kama ingekuwa kuamini vitu hivyo ndio kufanikiwa hata Harmonize nisingekutana naye, nilivyokutana na Harmonize na kuanza kuimba sikuwa nafanya hivyo vitu kwanini nifanye sasa hivi?..sijawahi kujua faida yake,” alisema Ibraah.
Pamoja na hayo ameweka wazi mambo kadhaa kuhusu muzuki wake ikiwa ni pamoja na album ya ‘The king of new school’ ambayo ameiachia wiki chache zilizopita ikiwa ndio album yake ya kwanza tangu kuingia kwake rasmi kwenye tasnia ya mzuiki wa Bongo fleva.
Kumekuwa na wimbi la watu wanaoamni kuwa Wanamuziki hawafanikiwi mpaka waende kwa waganga na kuwa sanaa ya muziki ni kinara ya masuala ya namna hiyo.