Siku ya jana mahakama jijini Barcelona nchini Uhispania iliamuru kufanyika kwa uchunguzi wa mwili wa Rais huyo kutokana na maombi ya binti yake aitwae Tchize dos Santos, ambaye alisema kuwa ana wasiwasi na kifo cha baba yake kwamba huenda kimesababishwa na mauaji.
Bw. Dos Santos alifariki dunia katika hosptali ya Barcelona ijumaa iliyopita alipokua akiendelea na matibabu.
Mwanasheria wa familia hiyo amekataa madai ya serikali kutaka mwili wa mwanasiasa huyo wa muda mrefu kuletwa nchini Uhispani kwa ajili ya maziko, na badala yake ufuatwe wosia alioacha kuwa, endapo atafariki dunia azikwe nchini Uhispania tena na familia yake pekee.
Serikali ya nchi hiyo inataka mwili huo urejeswe Angola ili uzikwe kitaifa.