Imeisha Hiyo! Hatimaye Klabu ya Yanga Rasmi Yamtambulisha Aziz Ki Usiku Mnene




Kiungo mshambuliaji Burkina Faso, Stephane Aziz Ki akiwa na Rais wa Yanga Injinia Hersi Said
Kiungo mshambuliaji  Raia wa Burkina Faso, Stephane Aziz Ki (26) hatimaye ametangazwa rasmi kuwa mchezaji wa klabu ya Yanga kabla ya kujiunga na Yanga, Aziz Ki alikuwa akiichezea klabu ya soka ya Asec Mimosa ya huko Ivory Coast.

Nyota huyo ambaye utambulisho wake ulikuwa unasubiriwa kwa hamu na wapenzi na mashabiki wa Yanga ametambulishwa usiku wa kuamkia leo.

Aziz Ki amewahi kuchezea klabu mbalimbali ikiwemo San Roque (2015-2016), Omonia (2017-2018) pamoja na Nea Salamis (2018- 2019), Stephane Aziz Ki ameichezea klabu ya Asec Mimosa kwa misimu miwili kabla ya kujiunga na Klabu ya Yanga.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad