Inauma..Mtoto Mmoja Kati ya Mapacha Waliotenganishwa Muhimbili Afariki Dunia


Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa masikitiko imetoa taarifa ya kifo cha Mtoto Neema ambaye alitenganishwa na mwenzake Rehema, Neema amefariki Jumapili ya tarehe 10 Julai saa 3 asubuhi.

“Akiwa ICU hali yake ilibadilika ghafla, Madaktari walijitahidi kurudisha hali yake bila mafanikio na hatimaye kupoteza maisha, tuendelee kumwombea Rehema ambaye bado yupo ICU ili Mwenyezi Mungu amjalie afya njema, Bwana alitoa na Bwana ametoa, jina lake lihimidiwe sana”

Upasuaji wa kuwatenganisha Watoto waliokuwa wameungana (Neema na Rehema) ulifanyika July 01,2022 kwa mafanikio katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambapo Jopo la Wataalamu 31 walitumia saa saba kukamilisha upasuaji huo.

Watoto hao mapacha wawili wenye umri wa miezi tisa walizaliwa wakiwa wameungana sehemu ya kifua na tumbo na kwa upande wa umbo la ndani wameungana ini ila kila Mtoto ana ini lake.

Tanzania imekuwa nchi ya tatu Barani Afrika kufanya upasuaji wa aina hii baada ya Afrika ya Kusini na Misri.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad