Jamaa Anayekula Mchele Kilo 10, Mbuzi Mzima Pekee yake Asema Mkewe Alimtoroka




Mwanamume Mtanzania mwenye uwezo wa kula kilo 2 za wali na mbuzi mzima kwa wakati mmoja amefichua kuwa mkewe alimuacha kwa kula sana.



Saidi Msosi ambaye hivi majuzi alishinda shindano la Tonge nyama mjini Morogoro, aliwaacha watu vinywa wazi baada ya kumaliza mandazi 40 ndani ya dakika 20 pekee.

Katika mahojiano na Millard Ayo, Msosi alisema alimtembelea daktari na kuambiwa kuwa ana tumbo kubwa sana tofauti na watu wa kawaida na anatakiwa aendelee kula zaidi.

Magazetini Julai 11: George Wajackoyah Ajenga Ikulu yake ya Vyumba 3 Kijijini
“Nimetoka kula mandazi 40 ndani ya dakika 20. Nilianza kula sahani tatu hadi nne hadi nilipofika ngazi za juu,” alisema Msosi.


 
“Nilikwenda kuangalia nikaambiwa tumbo ni kubwa sana,” aliongeza.

Mkewe alikimbia kwenye milima ya karibu alipoona jinsi mwanamume huyo anavyokula na pia alichoka kupika chakula kingi.

Nyumbani kwake, anakula kilo 3 za wali na kuku wawili mzima katika mlo mmoja, kila siku.


“Mimi ni mseja, naajiri tu vijana wa kunipikia, kisha kuwalipa fedha, kwa sasa nipo singo, sitaki mwanamke mwingine,” alisema Msosi.

Kwa sasa, anaweza kula kilo 10 za wali na mbuzi mzima katika mlo mmoja.

Msosi ametengeneza pesa nyingi kutokana na mashindano ya kula na anamiliki ploti, nyumba na pikipiki mbili

Msosi mwenye uzito wa kushangaza wa kilo 72, alikanusha madai kuwa anatumia uchawi kushinda mashindano hayo.


 
Nairobi: Mwanaume Aliyefuzu na Shahada ya Uzamili Achuuza Mayai Barabarani
Ugali man
Ugali man ambaye anakula kilo 2 za ugali kila siku amelalamikia kupanda kwa gharama ya maisha na anataka bei ya bidhaa muhimu kupunguzwa.

Charles Odongo, aliibuka maarufu mtandaoni baada ya video yake akirusha ugali hewani kusambaa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad