Kajala wa Harmonize Aanza Kazi Rasmi Konde Gang..Ukimtaka Harmonize Sharti Upitie Kwake


Supastaa @kajalafrida ambaye ni meneja wa mwanamuziki @harmonize_tz ametangaza rasmi ratiba ya shows za mkali huyo mwezi huu wa Julai.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Kajala amebainisha kuwa usiku wa leo, Harmonize atakuwa na show huko Doha nchini Qatar huku zingine zitakazo kamilisha mwezi huu ni pamoja na ya Dubai, Julai 16 na ya Mtwara, Julai 23.

"More Booking Contact me Let’s Go" - aliongeza Kajala ambaye kasafiri na Harmonize, kwenye maelezo yake.

Ikumbukwe, Kajala alitambulishwa rasmi kuwa mkurugenzi na meneja wa msanii Harmonize, Juni 6, mwaka huu. Na taarifa hiyo iliyotolewa na Choppa ambaye pia ni mmoja wa mameneja wa Harmonize.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad