Kijana Afariki Dunia Baada ya Kunywa Chupa Nzima ya Jägermeister Akishindana na Wenzake Kunywa Pombe


Kijana mmoja (miaka kati ya 25 na 30) Raia wa South Africa ameripotiwa kufariki baada ya kunywa chupa nzima ya pombe aina ya Jägermeister kwa kugugumia chini ya dakika mbili katika shindano la unywaji pombe kupita kiasi huko Waterval, Limpopo Afrika kusini, mitandao ya Nchi hiyo imeripoti.

Kwenye video iliyosambaa kwenye mitandao kijana huyo anaonekana akiifakamia chupa hiyo huku Watu wakimpigia makofi na kumshangilia ambapo Polisi wa Limpopo wamesema tukio hili limetokea katika kituo cha kuuza pombe za kienyeji ambapo Wateja walishiriki katika shindano la unywaji pombe lililokuwa na zawadi ya Randi 200 ambazo ni sawa na Tsh 27,625.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad