Kitambulisho NIDA kikiisha muda kitaendelea kutumika




Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida) imewataka wananchi wenye vitambulisho vya taifa ambavyo muda wake wa matumizi unaisha mwakani kutokuwa na hofu kwa sababu kinachoisha muda ni kitambulisho kama kasha tu, lakini taarifa za utambulisho wa mtu ziko pale pale na zitaendelea kutumika.

Aidha, imesema namba ya utambulisho wa mtu mwenye kitambulisho hicho itaendelea kuwa ileile na kuwataka wananchi waondoe hofu iliyotanda kuwa utambulisho wao unapotea kitambulisho kinapoisha muda wa matumizi.

Akizungumza jana katika Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam yanayoendelea Dar es Salaam, Msemaji wa Nida, Geofrey Tengeneza alisema kumekuwa na maswali mengi na hofu miongoni mwa jamii kuwa vitambulisho vya taifa vilivyotolewa mwaka 2012 ambavyo vinaisha muda wake mwakani kuwa taarifa zao zitapotea.

“Kwanza niwaondoe hofu wananchi, ni kweli kuwa vitambulisho vya taifa ambavyo vilianza kutolewa mwaka 2012 muda wake wa matumizi unaisha mwakani, lakini kinachoisha ni gamba tu kama ambavyo leseni ya udereva ina expire (kuisha muda), lakini taarifa za mtu hazipotei zinaendelea kutumika, hiyo ni sambamba na namba yake ya Nida,” alisema Tengeneza.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad