Kocha Mpya Simba Atoa Msimamo




KOCHA Mkuu wa Simba, Zoran Manojkovic, amesema hajali sana suala la matokeo katika mechi yao ya kirafiki kwa sababu anahitaji kuona aina ya timu yake kwa ajili ya kuimarisha msimu mpya wa 2022/23.

KOCHA Mkuu wa Simba, Zoran Manojkovic.
Simba juzi ilicheza mechi ya kwanza ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Ismailia FC, na kutoka sare ya 1-1 mchezo uliopigwa katika dimba la Ismailia, nchini Misri.

Bao la Simba likifungwa na Augustine Okrah ikiwa ni bao lake la kwanza tangu alipojiunga na klabu hiyo kwa msimu huu wa mashindano.

Akizungumza na gazeti hili jana, Zoran alisema mechi wanazocheza kwa ajili ya kuona na kupata mwanga wa kikosi chake na ana imani baada ya mechi nne zijazo zitamsaidia kufanya vizuri zaidi.

Alisema hajalishi matokeo anayoyapata zaidi ya kuhitaji kuona timu yake inapata michezo ya kirafiki kwa kuona upungufu na uwiano wa wachezaji wake.


“Ni kweli tumecheza mechi ya kirafiki matokeo sio muhimu sana kwa sababu nahitaji kuona wachezaji wangu licha ya wachezaji kutokamilika wote, nina imani mechi zijazo zitatusaidia kufanya vizuri zaidi,” alisema Zoran.

Katika hatua nyingine Ahmed Ally alisema klabu imefika makubaliano ya kumwongezea mkataba mpya wa miaka miwili kiungo mkabaji wao, Mzamiru Yassin.

Alisema kupitia ripoti ya mwalimu amerishishwa na kiwango cha kiungo huyo kupewa mkataba mpya kutumikia timu hiyo kwa msimu ujao.


“Mzamiru atakuwapo katika kikosi cha Simba, tunaendelea kukiimarisha kikosi ikiwamo kuongeza mikataba ya wachezaji ambao tunaamini bado ni msaada mkubwa kwetu," alisema Ahmed Ally.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad