Mabao Bora Yaliyotikisa Ligi Kuu Tanzani 2021/22



MSIMU ulimalizika jana lakini yalifungwa mabao bora kwenye michezo mbalimbali yaliyowavutia watazamaji kama ambavyo, nakudondolea;

Anaingia kwenye vitabu vya kumbukumbu akifunga bao la kwanza msimu huu dhidi ya Mtibwa Sugar kwa shuti kali na kuiwezesha timu yake kushinda bao 1-0, mchezo uliopigwa Septemba 27, 2021, kwenye Uwanja wa Mabatini.

CRISPINE NGUSHI (MBEYA KWANZA)

Anaichezea Yanga kwa sasa ila anakumbukwa kwa bao kali la pili alilofunga kwa mtindo wa ‘Tikitaka’ dhidi ya Mbeya City ulioisha kwa sare ya mabao 2-2, Oktoba 3, mwaka jana na kumsababishia kadhia baada ya kuzimia.

EMMANUEL MARTIN (DODOMA JIJI)

Bao la ushindi wa 2-1, alilofunga kutoka kwa Tanzania Prisons Oktoba 24, mwaka jana linaingia pia kwenye mabao makali yaliyofungwa msimu huu kutokana na umaridadi mkubwa aliotumia kufunga kwa kichwa cha kuzamia.


CRISPINE NGUSHI (MBEYA KWANZA)

Bao la kichwa alilofunga kwenye mchezo na Polisi Tanzania ulioisha kwa mabao 2-2, Novemba Mosi 2021, ni moja ya bao bora kufunga.

FEISAL SALUM ‘FEI TOTO’ (YANGA)

Unapozungumzia mabao bora hutoacha la kiungo wa Yanga, Feisal Salum ‘Fei Toto’ alilowafunga Ruvu Shooting Novemba 2, 2021, katika Uwanja wa Benjamin Mkapa kwa shuti kali nje ya eneo la 18 na Yanga ikishinda 3-1.

MEDDIE KAGERE (SIMBA)

Bao alilowafunga Namungo Novemba 3, mwaka jana linaingia kwenye miongoni mwa mabao bora kutokana na jitihada zake binafsi za kupiga kichwa kikali mbele ya mabeki dakika za mwisho na kuiwezesha timu yake kushinda 1-0.


CHARLES ZULU (AZAM FC)

Nyota huyu ingizo jipya kwenye kikosi hicho, anakumbukwa pia kwa bao kali alilowafunga KMC, Novemba 21, 2021 kwa shuti kali nje ya eneo la 18, licha ya timu yake kufungwa 2-1, mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Uhuru.

RICHARD NG’ONDYA (MBEYA CITY)

Bao la pili alilofunga kwenye mchezo dhidi ya Azam Desemba 18, 2021, uliomalizika kwa timu hizo kufungana 2-2, linaingia pia katika mabao bora ya msimu huu kutokana na kupiga Frii-Kiki zuri sana nje ya eneo la 18.

NEVER TIGERE (AZAM FC)

Bao la pili alilofunga kwenye mchezo dhidi ya Mbeya City Desemba 18, 2021, na kuisha kwa timu hizo kufungana 2-2, linaingia pia katika mabao bora ya msimu huu kutokana na kupiga Frii-Kiki kali sana nje ya eneo la 18.

TEPSI EVANS (AZAM)

Bao alilowafunga Ruvu Shooting Desemba 23, 2021 kwenye ushindi wa timu hiyo wa mabao 4-1, katika Uwanja wa Azam Complex Chamazi ni miongoni mwa mabao bora kutokana na umbali aliopiga akiwa pembeni mwa uwanja huo.


KIBU DENIS (SIMBA)

Bao la nne alilowafunga KMC nje ya 18 kwenye ushindi wa 4-1, Desemba 24, 2021 katika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi Tabora ni moja ya mabao bora kufungwa.

FISTON MAYELE (YANGA)

Husifika kwa aina ya kushangilia kwa mtindo wa ‘Kutetema’ na bao lake la ‘Tikitaka’ alilowafunga Biashara United Desemba 26, mwaka jana linakuwa miongoni mwa mabao bora yaliyofungwa wakati timu yake ikishinda 2-1.

RODGERS KOLA (AZAM)

Nyota huyo alifunga bao kali dhidi ya Simba Januari Mosi, 2022 akitokea benchi licha ya timu yake kupoteza mabao 2-1.

CLATOUS CHAMA (SIMBA)

Alifunga bao la kikatili wakati alipowahadaa mabeki wa Biashara United katika mchezo uliopigwa Machi 4, 2022 na kuiwezesha timu yake kushinda mabao 3-0, mechi iliyopigwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam.


RASHID CHAMBO (COASTAL UNION)

Aliingia kipindi cha pili wakati wa mchezo dhidi ya KMC uliopigwa Machi 7, 2022 na kupiga shuti kali nje ya 18 dakika za mwishoni na kuipatia timu yake ushindi wa 3-2, katika mchezo uliopigwa Uwanja wa Azam Complex.

FISTON MAYELE (YANGA)

Aprili 6, mwaka huu katika Uwanja wa Azam Complex, Mayele alipiga bao kali la ‘Tikitaka’ na kuiwezesha timu yake kushinda mabao 2-1.

HAMIS KANDURU (MBEYA KWANZA)

Bao lake la kwanza kwenye ushindi wa 2-0, dhidi ya Coastal Union April 22, 2022, linakuwa bao bora kufungwa msimu huu.

WILLIAM EDGAR (MBEYA KWANZA)

Bao lake la pili kwenye ushindi wa 2-0, dhidi ya Coastal Union April 22, 2022, linakuwa bao bora kufungwa na nyota huyo kutokana na jinsi alivyotoka katikati mwa uwanja hadi kufunga dakika ya mwisho kabisa ya mchezo.

SAMSON MADELEKE (MBEYA CITY)

Bao la kichwa alilolifunga katika mechi dhidi ya Dodoma Jiji waliopoteza mabao 2-1, mchezo uliopigwa April 23, 2022 katika Uwanja wa Jamhuri Dodoma linaingia kwenye mabao bora msimu huu kutokana na jitihada binafsi.


SHIZA KICHUYA (NAMUNGO FC)

Kichuya amekuwa kwenye kiwango bora msimu huu akiwa na timu hiyo na bao lake linalokumbukwa zaidi ni dhidi ya Yanga April 23, 2022, kwa shuti kali lililomshinda kipa, Djigui Diarra licha ya wao kufungwa mabao 2-1.

DICKSON AMBUNDO (YANGA)

Mei 15, 2022 wakati Yanga inashinda 2-0, dhidi ya Dodoma Jiji katika Uwanja wa Jamhuri, alipiga shuti kali lililomshinda kipa Mohamed Yusuph ambaye baada ya kufungwa bao la kwanza alijikuta akijifunga mwenyewe bao la pili.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad