IRENE Uwoya mwenyewe anajiita Pisi Kali; ni supastaa wa Bongo Movies mwenye pesa zake ambaye hivi karibuni ametoa tuhuma nzito dhidi ya wanafunzi wanaosomea udaktari wa binadamu.
Kama kawaida yake, Uwoya huwa anatoa nukuu zake kadha wa kadha, lakini nukuu hii; “Jitahidini kula vizuri na kufanya mazoezi sana, madaktari wenu wa baadaye hawahudhurii vipindi huko vyuoni…” imeleta gumzo baada ya wanafunzi hao wa udaktari kumcharukia.
Baadhi ya maoni juu ya kauli hiyo ni haya; “Hii kauli kwamba wanaosoma udaktari hawahudhurii vipindi ni dharau kubwa sana, Uwoya amejuaje?
“Amefanya utafiti gani kugundua kwamba wanafunzi wa udaktari ni madoja?
“Kama amefanya utafiti wake atangaze mbele ya vyombo vya habari na atoe vielelezo vyote, maana kama hujafanya utafiti ni bora ukae kimya tu.
“Kauli ya Uwoya imemaanisha mengi, mojawapo ni kwamba haamini uwezo wa madaktari.
“Wanafunzi wa udaktari na madaktari hivi mmeichukuliaje hii kauli?
“Yani mtu kakurupuka tu kazi yake hata haijulikani halafu anapata ujasiri wa kupondea taaluma ya Udaktari….”